
Shambulizi hilo lililofanywa kwa usaidizi wa washirika wa kijeshi wa Marekani limezilenga ngome za IS kote nchini Syria. Jeshi la Jordan lilitangaza kushiriki katika mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo ya jana Jumamosi ni sehemu ya hatua ya kujibu mapigo iliyochukuliwa na rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya shambulizi la ISIS lililomuua sajenti Edgar Brian Torres-Tovar, sajenti William Nathaniel Howard, na Ayad Mansoor Sakat, katika eneo la Palmyra.
Marekani imeendelea kusema kwamba inatoa ujumbe mzito kwa yeyote atakayewadhuru wapiganaji wa Marekani kwamba watatafutwa na kuuawa kokote pale walipo.
Siku moja kabla ya shambulizi hilo afisa mmoja wa Syria alisema vikosi vya taifa hilo vimemkamata kiongozi wa operesheni za IS.