
Baada ya ziara za viongozi waliopita, sasa Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz anatarajiwa kuzuru India kuanzia Januari 11 hadi 13, ambapo atakutana na Waziri Mkuu Narendra Modi katika jimbo la Gujarat na baadaye kuzuru Bangalore kukutana na wawakilishi wa kampuni za Ujerumani.
Ziara hiyo inaambatana na ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara, ikionyesha uzito wake wa kiuchumi.
Katika dunia inayozidi kuwa na misukosuko ya kisiasa na kiusalama, Ujerumani inatafuta washirika wapya wa kuaminika, hasa wakati mshirika wake wa jadi, Marekani, ameanza kuchukua hatua zinazotia wasiwasi kama vitisho dhidi ya Greenland na ushuru mkubwa kwa bidhaa za Ulaya.
Ujerumani inaiona India kama mshirika muhimu kwa sababu ya ukuaji wake mkubwa wa kiuchumi (wa zaidi ya asilimia sita), tofauti na Ujerumani inayokabiliwa na mdororo wa uchumi.