Ijumaa, viongozi wa vyama vya siasa vya Greenland walisema, “Hatutaki kuwa Wamarekani, hatutaki kuwa Wadenmaki, tunataka kuwa Wagrinlandi,” kufuatia matamshi ya Trump yaliyonyesha nia ya kuchukua Greenland.

Akiwa katika tukio Ikulu Ijumaa, Trump alisema, “Tutafanya kitu kuhusu Greenland, wapende wasipende kwa sababu ikiwa hatutafanya, Urusu au China watachukua Greenland, na hatutaki Urusi au China kama jirani.” Aliongeza, “Ningependa kufanya mkataba kwa njia rahisi, lakini kama hatutafanya kwa njia rahisi, tutafanya kwa njia ngumu.”

Matamshi ya Trump yamepata lawama, huku nchi za Ulaya hasa zikitahadharisha kwamba hatua kama hiyo inaweza kumaanisha mwisho wa NATO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *