
Mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wa xa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yanaongezeka nchini Hamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Umoja wa Mataifa unaonya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA), imetoa ripoti mpya: Matukio 626 yaliathiri wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu kote nchini mwaka 2025. Na hali inazidi kuwa mbaya. Mwishoni mwa mwaka, matukio 48 yalirekodiwa mwezi Desemba pekee Mashariki mwa nchi. Barabara kukatika, uwepo wa makundi yenye silaha, wizi, na vitisho, kutoa misaada ya kibinadamu inakuwa kazi hatarishi.
Kati ya matukio 48 yaliyorekodiwa mwez Desemba 2025 mashariki mwa DRC, nusu yalitokea katika mkoa wa Kivu Kusini, kulingana na OCHA, Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Hii inawakilisha visa kumi zaidi ikilinganishwa na mwezi Novemba, shirika hilo linaongeza.
Mkoa wa Kivu Kaskazini unafuata, Ukifuatiwa na mkoa wa Ituri. Kwa Umoja wa Mataifa, ongezeko hili linaonyesha kuzorota zaidi kwa mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu, hasa katika mkoa wa Kivu Kusini, mwishoni mwa mwaka, katika muktadha wa mapigano na ukosefu wa usalama ulioenea.
Hasa, matukio haya mara nyingi ni wizi, mashambulizo na uvamizi. Lakini wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu pia wanakabiliwa na vitisho, vikwazo na wakati mwingine hata mashambulizi. Matokeo yake, shughuli zinapungua, na baadhi ya watu ni vigumu zaidi kuwafikia.
Licha ya matukio hayo kurekodiwa kwa weingi mwezi Desemba huko Kivu Kusini, Kivu Kaskazini inabaki kuwa mkoa uliloathiriwa zaidi kwa mwaka wa 2025, ikishughudia 46% ya matukio. Ni eneo ambalo ukosefu wa usalama unaendelea kuwa kwa kiwango cha juu, ambapo maeneo ya vita yanabadilika, na ambapo wafanyakazi wengi wa mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu wapo, jambo ambalo bila shaka huongeza hatari.