
Araghchi amesema hayo kama jibu kwa vitisho vya rais wa Marekani Donald Trump kwamba atashambulia Iran kijeshi kufuatia hatua ya jamhuri hiyo ya Kiislamu kukandamiza waandamanaji, ambapo watetezi wa haki za binadamu wameripoti kwamba mamia wameuawa.
Kwa wiki mbili zilizopita, maandamano ambayo awali yalichochewa na hali ngumu ya uchumi, yamegeuka kuwa ya vurugu na miongoni mwa mitihani mikubwa kwa utawala wa Iran ambao umedumu tangu mapinduzi ya kiislamu ya mwaka 1979.
Rais Donald Trump amesema mkutano na viongozi wa Iran unaandaliwa, lakini pia atatafakari hatua za kijeshi.
Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amelaani ukandamizaji dhidi ya maandamano ya amani Tehran.
Umoja wa Ulaya umesema unatafakari kutangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa Iran kuhusu ukandamizaji huo wa waandamanaji.
China kwa upande wake imesema inapinga ‘uingiliaji’ wa mambo ya Iran.