Myanmar inakabiliwa na tuhuma za mauaji ya halaiki dhidi ya jamii ndogo ya Warohingya, katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) ya Umoja wa Mataifa iliyoko The Hague Uholanzi.

Gambia ilifungua kesi kwa mara ya kwanza dhidi ya Myanmar, mnamo mwaka 2019 ikidai kuwa “operesheni ya kusafisha” iliyofanywa na jeshi la Myanmar mwaka 2017 ilikiuka Mkataba wa kuzuia Mauaji ya Kimbari wa mwaka 1948.

Wakati wa operesheni hiyo, vikosi vya serikali vilituhumiwa kwa kadhia mbalimbali ikiwemo ubakaji wa watu wengi na kuchoma maelfu ya nyumba za watu. Takriban watu 700,000 wengi wakiwa wa jamii ya Rohingya, walilazimika kuyakimbia makaazi yao.

Lucky Karim ambaye ni afisa wa shirika linalotetea haki za Warohingya amesema kesi ya Myanmar katika mahakama ya ICJ inatoa mwanga wa matumaini kwa mamia ya maelfu ya watu akiwemo yeye na kwamba jitihada zao za kutafuta haki hazitapuuzwa,”

Hata hivyo Myanmar ambayo inatawaliwa kijeshi imekanusha mashtaka dhidi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *