
Nchini Mali, kizuizi cha kiuchumi kilichowekwa kwa mafuta mwezi Septemba mwaka uliyopita na wanajihadi kimeenea hadi kwenye vituo vya viwanda. Viwanda vya wafanyabiashara wa Mali na India vimeshambuliwa siku ya Jumapili, Januari 11, na washukiwa kutoka makundi ya wanajihadi wanaohusishwa na Al Qaeda katika eneo la Kayes magharibi mwa Mali.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel
Vituo vitatu vya viwanda vililengwa mapema siku ya Jumapili asubuhi, Januari 11, na washukiwa kutoka makundi ya wanajihadi wanaohusishwa na Al Qaeda. Vituo hivi vinazalisha saruji, chokaa, na plasta katika eneo la Kayes magharibi mwa Mali. Washambuliaji walifika eneo hilo wakiwa na pikipiki, wakiwa na silaha nzito. Kulikuwa na watu wenye silaha kati ya 150 na 200 kulingana na vyanzo mbalimbali. Wakiwa wamegawanywa katika makundi mawili, walishambulia na kuchoma viwanda hivyo vitatu.
Matukio yaliyorekodiwa yalishirikiwa kwenye mitandao ya kijamii. Afisa aliyechaguliwa wa eneo hilo alitembelea eneo la tukio baada ya wanajihadi kuondoka. Alielezea hali ya kutisha: mifuko ya saruji iliyochomwa, majengo yaliyoharibiwa, na uharibifu mkubwa wa vifaa mbalimbali. “Kila kitu lazima kijengwe upya,” chanzo kingine katika mji wa Bafoulabé kimetuambia, huku kikimeongeza kuwa “wanajihadi hawataki tena viwanda hivyo kufanya kazi.”
Kulingana na taarifa zetu, angalau watu wanne walitekwa nyara kutoka katika moja ya maeneo matatu yaliyoshambuliwa. Mwezi Julai mwaka uliyopita, wanajihadi walishambulia viwanda katika eneo hilo. Wafanyakazi wa kigeni, wakiwemo Wahindi, walitekwa nyara. Bado wanashikiliwa na kundi moja lenye silaha linaloshirikiana na Al Qaeda.