Waziri mkuu wa Sudan, Kamil Idris ametangaza shughuli za serikali kurejea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum, baada ya miaka mitatu ya kuwa inaendesha shughuli zake huko Port Sudan.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari siku ya Jumapili, amesema serikali imerejea rasmi mjini Khartoum na itaanza juhudi za kuboresha huduma kwa wakazi wa mji huo.

Idris amesema serikali itafanya kazi katika kuboresha umeme, maji, huduma za afya na elimu ambapo pia alitangaza kuwa mwaka 2026 utakuwa “mwaka wa amani” kwa Sudan, wakati huu watu takriban laki moja na Elfu 50 wakiwa wameuwa tangu vita vilipozuka mwaka 2023.

Umoja wa Mataifa umeitaja hali hiyo kuwa janga baya zaidi la kibinadamu duniani na takriban watu Milioni 12 wamelazimika kuyahama makazi yao.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamewashutumu wapiganaji wa RSF pamoja na wanajeshi wa serikali kutekeleza vitendo vya ukatili, mauaji na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *