Tahadhari yatolewa kuhusu mauaji ya halaiki IranTahadhari yatolewa kuhusu mauaji ya halaiki Iran

Maafisa wa mamlaka za Iran wamefanya “mauaji ya halaiki” katika kukandamiza maandamano makubwa zaidi dhidi ya jamhuri ya Kiislamu kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka mingi.

Hayo yamesemwa na kundi la haki za binadamu jana Jumapili, huku serikali ikiamuru maandamano ya kujibu ili kurejesha utulivu.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Iran lisilo la kiserikali Iran Human Rights (IHR) lenye makao yake makuu nchini Norway lilisema limethibitisha mauaji ya waandamanaji wasiopungua 192 lakini likaonya kwamba idadi halisi ya vifo inaweza kufikia mamia kadhaa, au hata zaidi. 

Kwa mujibu wa kundi la haki za binadamu lenye makao yake makuu Marekani, takriban waandamanaji 490 na wanajeshi 48 wameuawa.

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kufanya mkutano na maafisa wake wakuu kesho Jumanne, kujadili njia za kujibu maandamano nchini Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *