Watu wenye silaha walivamia mashua yenye uvuvi Pwani ya Gabon na kuwateka, wapiga makasia tisa, kwa mujibu ya Wizara ya Ulinzi nchini humo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita, katika ukanda wa Pwani, unaokwenda Senegal hadi Angola, eneo ambalo limekuwa likishuhudia uharamia.

Ripoti zaidi zinasema, wapiga makasia waliotekwa ni pamoja na raia watano wa China na wanne kutoka Indonesia.

Mashua hiyo yenye maandishi IB Fish 7, iliyokuwa na bendera ya Gabon, ilikuwa kwenye shughuli za uvuvi, Kusini Magharibi mwa Bahari wakati, ilipovamiwa.

Mwezi Februari mwaka uliopita, wapiga makasia wengine watatu walitekwa na watu wenye silaha, wakati wakivua samaki.

Eneo la Bahari ya Atlantic, katika eneo la Guba ya Guinea, ni barabara kuu ya mafuta na gesi kutoka mataifa ya Afrika Magharibi.

Licha ya matukio ya uharamia kupungua, katika miaka ya hivi karibuni, kwa sababu ya operesheni ya kiusalama kati ya mataifa ya Afrika na yale kutoka barani Ulaya, kuna visa vya mara moja moja vinavyowalenga wavuvi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *