Rais wa Cuba Miguel Díaz-Canel alisema Jumatatu kwamba utawala wake hauko kwenye mazungumzo na serikali ya Marekani, siku moja baada ya Rais Donald Trump kutishia kisiwa hicho cha Karibik kufuatia shambulizi la Marekani dhidi ya Venezuela.

Díaz-Canel alichapisha taarifa nyingi fupi katika mtandao wa kijamii wa X baada ya Trump kupendekeza Cuba “ifanye makubaliano, kabla haijachelewa. Hata hivyo hakusema ni aina gani ya makubaliano.

Díaz-Canel aliandika kwamba ili “uhusiano kati ya Marekani na Cuba uendelee, lazima utegemee sheria ya kimataifa badala ya uadui, vitisho, na kulazimishwa kiuchumi.” Kauli zake zilichapishwa tena na Waziri wa mambo ya nje wa Cuba Bruno Rodríguez kwenye mtandao wa X.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *