Karibu matrekta kumi na tano ya FNSEA (Shirikisho la kitaifa la Vyama vya Wakulima) na wakulima vijana wameingia ktika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, leo Jumanne, Januari 13, muda mfupi kabla ya saa 12:00 asubuhi (saa za Ufaransa), mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP amesema. Walikuwa wa kwanza kufika katika msafara mkubwa unaotarajiwa kushuhudiwa matrekta mia kadhaa yakiingia katika mji mkuu huu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakiingia kupitia Porte Dauphine, matrekta hayo, yakisindikizwa na malori ya polisi wa kutuliza ghasia, yatapita katika barabara kuu za mjini Paris, ikiwa ni pamoja na Champs-Élysées, kabla ya mkutano katika Wizara ya Mambo ya Nje, Quai d’Orsay.

Hatua hiyo inaandaliwa na FRSEA Grand Bassin Parisien (Shirikisho la Kikanda la vyama vya wakulima la Bonde Kuu la Paris), chombo kinachozunguka eneo la Île-de-France na idara katika maeneo jirani, kudai “hatua halisi na za haraka” ili kutetea uhuru wa chakula.

Hatua hii inakuja siku chache tu baada ya msaada mkubwa kutoka Uratibu wa Vijijini na Shirikisho la Wakulima.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *