India yaishutumu Pakistan kwa kurusha droni ndani ya KashmirIndia yaishutumu Pakistan kwa kurusha droni ndani ya Kashmir

Mkuu wa jeshi la India ameituhumu Pakistan kwa kurusha droni katika eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India, eneo ambalo mataifa hayo mawili yenye silaha za nyuklia yalipigana kwa siku nne mwaka uliopita.

Jenerali Upendra Dwivedi amesema tayari wameiambia Pakistan kwamba hatua hiyo haikubaliki na kuitaka iachane nayo mara moja.

Ameongeza kuwa wakuu wa operesheni za kijeshi wa nchi hizo mbili wamezungumza mapema leo.

Wiki iliyopita, jeshi la India liliripoti kuona droni kadhaa zikivuka na kuruka juu ya vijiji vya mpakani vinavyodhibitiwa na India.

Jimbo la Kashmir, lenye idadi kubwa ya Waislamu, imegawanywa kati ya India na Pakistan tangu mwaka 1947 baada ya kupata uhuru kutoka Uingereza, na mataifa yote mawili yanadai jimbo hilo ni sehemu ya himaya yake.

India na Pakistan zilipigana kwa siku nne mwezi Mei mwaka uliopita baada ya New Delhi kuishutumu Islamabad kuhusika na shambulio lililoua watalii katika eneo la Kashmir—madai ambayo Pakistan ilikanusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *