Shambulio la kijeshi la Marekani ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini Venezuela na lililowezesha kutekwa kwa Kiongozi wa nchi hiyo Nicolas Maduro na mkewe lilizusha hali ya wasiwasi na tahadhari kwa viongozi wa Iran.

Tehran ikiwa ni mmoja wa washirika wa karibu wa Maduro, ambaye alisalia madarakani mwaka 2024 baada ya uchaguzi uliogubikwa na wizi wa kura na ambao ulitupiliwa mbali na Umoja wa Ulaya na hivyo kutomtambua Maduro kama kiongozi halali wa Venezuela.

Baada ya kukamatwa kwake katika operesheni ya kushtukiza ya makomandoo wa Marekani, Maduro hatimaye alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya New York na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Maandamano yafanyika kuikosoa Marekani

To view this video please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video

Hatua hii ya kushangaza ya Marekani, imeweka bayana kuwa utawala wa Rais Donald Trump uko tayari kuchukua hatua za kijeshi ili kuzipindua tawala zinazokinzana na Washington bila kujali sheria na kanuni za kimataifa, hatua ambayo inatoa onyo kwa mataifa mengine ya kimabavu.

Iran imetoa wito wa kuachiliwa kwa Maduro na mkewe ambao imesema wametekwa nyara, huku msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje akisisitiza kuwa “hakuna sababu ya kujivunia katika hili kwa kuwa ni kitendo kilicho kinyume cha sheria.

Iran na Venezuela zaunganishwa na adui wao

Ni vigumu kuyaelezea mahusiano kati ya Iran na Venezuela kwa misingi ya kawaida ya kidiplomasia. Venezuela ipo katika eneo la Karibiki na idadi kubwa ya raia wake ni Wakatoliki, huku Iran ikiwa katika Ghuba ya Uajemi na raia wake wengi wakiwa ni Waislamu. Viwango vya biashara kati nchi hizo mbili si vikubwa mno huku kukiwa hakuna safari za ndege za moja kwa moja kati ya Caracas na Tehran.

Marekani Jiji la New York 2026 | Maafisa wanawasindikiza Nicolás Maduro na Cilia Flores hadi Mahakama ya Shirikisho ya Manhattan
Hatua ya maafisa wa utekelezaji wa sheria ilimkamata Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe Cilia Flores kutoka kwenye helikopta, huku Maduro akielekea Mahakama ya Daniel Patrick Manhattan ya Marekani kwa ajili ya kusikiliza kesi kwa mara ya kwanza nchini Marekani.Picha: Adam Gray/REUTERS

Lakini mahusiano yao yaliimarika kutokana na kuwa na adui wa pamoja ambaye ni Marekani. Pia nchi hizo mbili zimeunganishwa na namna ya kukabiliana na vikwazo vya kimataifa katika muundo wa ulimwengu unaotawaliwa na Marekani. Katika miongo mitatu iliyopita, ukaribu wa kisiasa pamoja na sera zao za kuipinga Marekani vimewezesha kuibuka kwa mtandao mpana wa ushirikiano katika sekta ya mafuta, fedha, viwanda na usalama.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Iran Ismael Baghaei alisisitiza kuwa “uhusiano wao na nchi zote, ikiwa ni pamoja na Venezuela, unaendelea na unategemea kuheshimiana kwa pande zote na kwamba serikali ya Tehran inaendeleza mawasiliano na mamlaka ya Venezuela.

Hata hivyo, mzozo wa kisiasa nchini Venezuela unashuhudiwa katika wakati mgumu kwa Iran ambayo kwa zaidi ya wiki moja, inakabiliwa na maandamano ya kitaifa ambayo yamekuwa yakichochewa na kudorora kwa uchumi na mfumuko wa bei, ambapo waandamanaji wanadai kuwepo mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, na hivyo kuzidisha shinikizo kwa uongozi mjini Tehran ambao kwa upande wake unasema waandamanaji wanafadhiliwa na mataifa ya kigeni yenye nia mbaya kwa Iran.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *