
Katika mfumo wa uchaguzi nchini Uganda, kama ilivyo katika nchi nyingine yoyote ya kidemokrasia, rangi na alama za vyama ni msingi wa utambulisho wa kisiasa na upigaji kura, haswa katika nchi ambayo uelewa wa sheria za kupiga kura unaweza kutofautiana kati ya watu wa tabaka moja hadi jengine.
Kila chama kilichosajiliwa kina utambulisho wake wa kipekee unaotumika kwenye kampeni kwanza kuvutia wafuasi, lakini pili, kuwasaidia wapiga kura kutambua alama za vyama siku ya upigaji kura.
Kwa sababu kampeni za kutafuta kura zinalenga watu kutoka kila pembe ya nchi, mara nyingi sio wapiga kura wote wanaojua kusoma na kuandika au kusoma vizuri majina ya vyama kwenye kura, alama na rangi huwasaidia watu kutambua chama wanachokipenda njia rahisi.
Vidokezo hivi huonekana kwenye karatasi za kupigia kura, mabango ya kampeni, mavazi na bendera – na mara nyingi huwa na maana zaidi zinazohusiana na historia, dhamira au maadili ya chama.
Utambulisho wa vyama kwa rangi zao
1. National Resistance Movement (NRM) – Rangi ya njano katika mapambo na bidhaa za kampeni zikiwemo fulana, leso au khanga, suti, kofia, bendera za vyama na magari.
NRM ni chama tawala cha muda mrefu cha Uganda, kinachoongozwa na Rais Yoweri Museveni, madarakani tangu 1986. Alama ya basi inaonyesha maendeleo, uwezo wa kwenda mbele na ufanisi, ikionyesha msisitizo wa chama juu ya utulivu na uongozi wa muda mrefu.
