Nchini Uganda, wiki ya mwisho ya kampeni za wagombea inaendelea kabla ya uchaguzi wa urais na wa wabunge uliopangwa kufanyika siku ya Alhamisi, Januari 15. Kampeni hiyo inamalizika rasmi leo Jumanne jioni, Januari 13.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Yoweri Museveni, aliye madarakani kwa miaka 40, anakabiliana na mwanamuziki wa zamani na sasa kiongozi wa upinzani Bobi Wine katika uchaguzi kwa mara ya pili mfululizo. Siku ya Jumatatu, mkuu wa nchi wa Uganda alikuwa katika wilaya ya Kasese, magharibi mwa mbali mwa nchi, kwa moja ya kampeni zake za mwisho.

Magharibi mwa Uganda, mbele ya umati wa watu elfu kadhaa waliovaa rangi za njano za chama cha NR, chama tawala, rais Yoweri Museveni alitetea rekodi yake, haswa utulivu wa kisiasa uliorejeshwa nchini tangu alipoingia madarakani mwaka wa 1986, baada ya miongo kadhaa ya machafuko ya kisiasa.

“NRM ilikataa siasa za kikabila na kidini kwa sababu hazina maana na hazina umuhimu wowote. NRM ilikataa udini; ndiyo maana tuliunda chama chenye nguvu na tuliweza kujenga taasisi imara za kitaifa: jeshi, polisi, utumishi wa umma, na vingine. Ni kutokana na hili kwamba sasa tuna amani.”

Kutokana na wito wa upinzani wa kupiga kura ya maandamano, ukishutumu muda mrefu wa rais madarakani na mabadiliko ya utawala wake, rais, badala yake, aliangazia maendeleo ya kiuchumi ya nchi katika kipindi cha miaka 40 iliyopita.

“Ungeni mkono NRM katika chaguzi hizi ili tuweze kuendelea kusonga mbele. Kwa sababu kile NRM inachowaambieni si mazungumzo matupu tu; ni kuhusu mambo ambayo tumefanya, mambo unayoweza kuona. Katika siku mbili, uungeni mkono NRM ili tuweze kuimarisha yale ambayo tayari tumeyafanikisha.”

“Kulinda mali,” ni kauli mbiu ya kampeni ya rais huyo mwenye umri wa miaka 81, anayewania muhula wa saba, aambaye anatarajiwa kufanya kampeni yake ya mwisho jijini Kampala leo Jumanne, Januari 13.

Mkutano mgumu kwa mgombea mwenzake Bobi Wine

Bobi Wine alikuwa katika mji mkuu, Kampala, siku ya Jumatatu hii, Januari 12. Mikutano miwili ilipangwa, mmoja ukiwa umefutwa; kulingana na kiongozi wa upinzani, alizuiwa kuifanya. Hata hivyo, Bobi Wine alifanikiwa kuwakusanya wafuasi wake katika wilaya ya Aga Khan katikati mwa jiji. Akiwa amevaa fulana isiyopitisha risasi na kofia ya chuma, Bobi Wine aliwataka wafuasi wake kuendelea kuwa na umoja. Matamshi yake yalirekodiwa na Kenneth Lukwago Anderson wa Idhaa ya Kiswahili ya RFI.

“Mapambano ni magumu, lakini lazima tuendelea kuwa na umoja ili kuhakikisha ushindi wetu. Kampeni yetu imefanikiwa kuwaleta pamoja watu wengi, vijana kwa wazee, na lazima kabisa wabaki na umoja ili kukabiliana na vitisho vyovyote.” Raia wa Uganda wameonyesha uwezo wao wa kuungana chini ya bendera yetu ya taifa. Hii imemkasirisha Rais Museveni na kuonyesha jinsi anavyopinga umoja wa kitaifa. Lazima tumwambie aache machafuko na vurugu. Kampeni itamaliziika jioni ya Jumanne, Januari 13.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *