
Nchini Chad, jeshi limepelekwa kwa siku kadhaa katika eneo la Moyen-Chari, karibu na mpaka na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Siku ya Jumanne, Januari 13, makabiliano yalianza katika eneo hilo kati ya wanajeshi wa Chad na waasi wa MPRD. Vifo kadhaa viliripotiwa pande zote mbili.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko N’Djamena, Nadia Ben Mahfoudh
Makabiliano huko Korbol, kusini mwa Chad, yalianza mapema asubuhi siku ya Jumanne, Januari 13. Kulingana na Luc Beyam, Katibu Mkuu wa kundi la wasi la MPRD, vikosi vya jeshi “viliingia Korbol kupitia mji wa NĂ©ou.” Wajumbe watatu, manaibu wakuu wawili, na mkuu wa kitengo cha jeshi walitumwa katika eneo hilo kutoa muda wa mwisho. Lakini kundi la waasi liliwakamata na kuwashikilia.
Luc Beyam anadai kwamba jeshi limekuwa “likijaribu, tangu Jumamosi, kuwazingira wapianaji wa kundi hilo la kisiasa na kijeshi.” Hata hivyo, chanzo kilicho karibu na mamlaka kinadai kwamba shambulio la kuvizia lilifanywa na wapiganaji wa MPRD.
Mapigano yaliendelea siku nzima, na kusababisha vifo na majeraha kadhaa miongoni mwa jeshi la Chad na waasi. Ikiwasiliana na RFI, serikali ilikataa kutoa maoni kwa wakati huu. Lakini katibu mkuu wa MPRD anabainisha kwamba kuna “majeruhi zaidi upande wa wanajeshi wa Chad.”
Mapigano haya yanakuja baada ya miezi kadhaa ya mazungumzo kati ya mamlaka na MPRD kwa ajili ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani. Lengo: kuona kundi la waasi likiweka silaha zake chini.
Lakini Luc Beyam anaelezea kwamba, licha ya “nia yao ya kudumisha njia ya mawasiliano, serikali ya Chad haijakubali madai yetu yoyote.” Hasa, mahitaji ya kuondolewa kwa vikosi vya jeshi kutoka ukanda wa kusini. Kulingana naye, “mapigano haya yanalenga kutoa shinikizo ili MPRD itie sahihi kujisalimisha bila masharti.”
