Iran: Mazishi ya walinda usalama waliouawa katika maandamano yafanyikaIran: Mazishi ya walinda usalama waliouawa katika maandamano yafanyika

Malefu ya raia wa Iran wamejitokeza jijini Tehran kuhudhuria mazishi ya maafisa wa usalama 100 waliouawa wakati wa maandamano, wakati huu serikali ikisema kesi dhidi ya waandamanaji waliokamatwa zitaendelea kwa kasi, licha ya vitisho kutoka kwa Marekani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wakati Iran ikitoa kauli hiyo, rais Trump Donald Trump, ambaye anaunga mkono maandamano yanayoendelea, amesema Marekani itachukua hatua kali na yenye nguvu dhidi ya Iran iwapo, itawanyonga waandamanaji.

Onyo hili la Trump linakuja, wakati huu mashirika ya kutetea haki za binadamu, yakieleza kuwa waandamanaji zaidi ya 2,400, wameuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama tangu kuanza kwa maandamano hayo.

Trump ameendelea kuionya Iran kuwa Marekani itaingilia kati iwapo itaendelea kuwauwa waandamanaji.
Trump ameendelea kuionya Iran kuwa Marekani itaingilia kati iwapo itaendelea kuwauwa waandamanaji. via REUTERS – IRAN PRESS

Katika hatua nyingine, Balozi wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa Amir Saeid Iravani, kupitia barua aliyoituma kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, amemshtumu rais Trump kwa kuchochea maandamano yanayoendelea ili kuiyumbisha kisiasa nchi hiyo.

Maandamano nchini Iran yalianza mwezi Desemba mwaka uliopita, kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha kabla ya kugeuka na kuwa dhidi ya serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *