
MOROCCO; Morocco imetinga fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) baada ya kuitoa Nigeria katika mchezo wa nusu fainali kwa penalti 4-2 mchezo uliomalizika muda mfupi uliopita.
Hatua ya penalti ilikuja baada ya timu hizo kutoka 0-0 dakika 90 za kawaida na hata zilipoongezwa dakika 30 bado hazikufungana.
Morocco sasa itacheza fainali na Senefal Januari 18, 2026. Senegal imefuzu fainali kwa kuifunga Misri bao 1-0 mapema leo katika mchezo mwingine wa nusu fainali.
