Mohamed Salah na Sadio Mane kupambana tena nusu fainali AFCON 2025Mohamed Salah na Sadio Mane kupambana tena nusu fainali AFCON 2025

Ni kama fainali yenyewe, ila ni nusu fainali ikiwa marudio ya fainali ya AFCON 2021. Mafarao wanahitaji mafanikio baada ya ukame wa miaka 16 AFCON.

Baada ya kushinda mara tatu mfululizo 2010, Misri imemaliza katika nafasi ya pili mara mbili, 2017 walipofungwa na Cameroon na 2021 kwa Simba wa Teranga.

Kwa kile kinachoonekana kama pengine yakawa mashindano ya mwisho ya mshambuliaji Mohamed Salah, Misri inatarajia kuwa yatakuwa mazuri kumuaga na ushindi.

Salah ameshinda mataji mengi makubwa, ikiwemo Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini hajawahi kutia kunyanyua kombe la AFCON na ana hamu sana kufanikisha hilo kabla kutundika daluga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *