Rais Macron aonya kuhusu mpango wa Marekani kuchukua GreenlandRais Macron aonya kuhusu mpango wa Marekani kuchukua Greenland

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameonya kuwa, iwapo Marekani itafanikiwa kuchukua kisiwa cha Greenland kinachomilikiwa na Denmark, hatua hiyo itakuwa na matokeo mabaya.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Macron ameliambia Baraza lake la Mawaziri kuwa, kuingiliwa kwa uhuru wa taifa la Ulaya ukifanyika utakuwa na madhara yasiyofutika, huku akisisitiza kuwa Ufaransa itasimama na Denmark kuhusu uhalali wake wa kumiliki Greenland.

Wakati Macron akisema hayo, Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen, amesema huu sio wakati wa kujadili hatima ya kisiwa hicho, iwapo wakaazi watataka kujitenga na kujitawala.

Kiongozi huyo amesisitiza kuwa, haingii akilini kuwa na Greenland inayojitawala, wakati huu Marekani ikiapa kukichukua kisiwa hicho.

Wakuu wa kisiwa hicho, kinachomilikiwa na Denmark, wanatarajiwa kukutana katika Ikulu ya White House kujadili hatima ya Greenland.

Rais Donald Trump, amesisitiza kuwa Marekani inahitaji Greenland kwa sababu za kiusalama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *