Thailand: Zaidi ya watu 22 wafariki katika ajali kwenye reliThailand: Zaidi ya watu 22 wafariki katika ajali kwenye reli

Zaidi ya watu 22 wameripotiwa kufariki wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya mashine ya kunyanyua vitu vizito kwenye reli ya mwendo kasi nchini Thailand kuvunjika na kuangukia treni ya abiria.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mamlaka nchini humo, mashine hiyo ambayo ilikuwa ikitumika katika ujenzi wa reli hiyo mwendo kasi ilivunjika na kuangukia treni kaskazini Mashariki mwa Mji wa Bangkok.

Waziri Mkuu wa Anutin Charnvirakul  amesema ni lazima waliosababisha kutokea kwa mkasa huo wataadhibiwa vikali.

Aidha imeripotiwa kuwa treni hiyo ilipoteza mwelekeo baada ya kuangukiwa na mashine hiyo kabla ya kushika moto.

Waziri Mkuu wa Thailand amesema waliochangia kutoka kwa ajali hiyo watawajibishwa.
Waziri Mkuu wa Thailand amesema waliochangia kutoka kwa ajali hiyo watawajibishwa. REUTERS – Chalinee Thirasupa

Wizara ya uchukuzi ya Thailand imesema treni hiyo ilikuwa na abiria 195 na ilikuwa ikisafiri kutoka Bangoko kuelekea katika wilaya ya Ubon Ratchathani.

Mashine hiyo ya kunyanyua vitu vizito ilikuwa ikitumika katika ujenzi wa reli ya mwendo kasi nchini Thailand, Mradi unaoungwa mkono na China na unaolenga kuiunganisha Bangkok na Mji wa Kunming nchini China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *