
Mamlaka ya Iran ina “udhibiti kamili” wa hali usalama, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema siku ya Jumatano katika mahojiano na Fox News, baada ya maandamano ya zaidi ya wiki mbili ambayo yamekandamizwa vikali. “Sasa […] utulivu unatawala. Tuna udhibiti kamili” wa hali ya usalama, amekiambia kituo hiki cha habari cha Marekani, kulingana na dondoo kutoka kwa mahojiano yaliyorekodiwa siku ya Jumatano.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Siku ya Jumanne, Donald Trump aliwahimiza waandamanaji wa Iran kuendelea na harakati zao hadi watakapoipindua mamlaka, akiahidi kwenye mtandao wake wa Truth Social kwamba “msaada unakuja,” bila kutoa maelezo zaidi. Aliongeza kuwa atachukua hatua “kwa nguvu sana” iwapo waandamanaji watauawa.
Walinzi wa Mapinduzi watishia kujibu kwa “usahihi” dhidi ya mashambulizi ya Marekani na Israel
Iran iko tayari kujibu “kwa usahihi” kwa shambulio lolote kutoka Marekani au Israel, mkuu wa kikodi cha Walinzi wa Mapinduzi alionya siku ya Jumatano, akizituhumu nchi hizi adui kuwa nyuma ya harakati za maandamano zinazoikumba Jamhuri ya Kiislamu. Katika taarifa iliyonukuliwa na televisheni ya serikali, Mohammad Pakpour pia alimtuhumu Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuwa “wauaji wa vijana wa Iran.”
Ufaransa: mkutano wa dharura wa Baraza la Ulinzi umeitishwa Alhamisi asubuhi kujadili hali nchini Iran
Mkutano wa Baraza la Ulinzi, uliolenga hasa maandamano nchini Iran yakikandamizwa na mamlaka, umeitishwa haraka saa 2:00 asubuhi kwa saa za Paris siku ya Alhamisi katika Ikulu ya Élysée, kulingana na vyanzo kadhaa vinavyofahamu jambo hilo Jumatano. Mkutano huu wa Baraza la Ulinzi, utaoongozwa na Emmanuel Macron na kuwaleta pamoja mawaziri na viongozi wa kijeshi husika, unafanyika huku Donald Trump akiongeza uwezekano wa mashambulizi dhidi ya Iran.
Uingereza “imefunga kwa muda” ubalozi wake mjini Tehran
Uingereza “imefunga kwa muda” ubalozi wake nchini Iran, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uingereza ililiambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano. “Tumefunga kwa muda ubalozi wa Uingereza mjini Tehran; sasa utafanya kazi kwa nji ya video,” msemaji wa Ofisi ya Mambo ya Nje amesema, akiongeza kuwa ushauri wa usafiri “umesasishwa ili kuakisi mabadiliko haya ya kibalozi.”
Uhispania inawasihi raia wake kuondoka Iran
“Wahispania walioko Iran kwa sasa wanashauriwa kuondoka nchini humo kwa kutumia njia zote zinazopatikana,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Uhispania imesema katika taarifa mpya ya ushauri wake wa usafiri.
G7 inatishia Tehran kwa “hatua zaidi za vikwazo”
Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za G7 wanasema “wako tayari kuweka hatua zaidi za vikwazo ikiwa Iran itaendelea na ukandamizaji wake dhidi ya maandamano,” katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na Ufaransa, ambayo inashikilia urais wa G7. “Tuna wasiwasi mkubwa na idadi kubwa ya vifo na majeruhi iliyoripotiwa. Tunalaani matumizi ya makusudi ya vurugu na ukweli kwamba waandamanaji wanauawa, wanazuiliwa kiholela, na wanafanyiwa mbinu za vitisho na vikosi vya usalama,” walisema mawaziri wa mambo ya nje wa Ujerumani, Canada, Marekani, Ufaransa, Italia, Japan, na Uingereza, pamoja na Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya.