.

Chanzo cha picha, Reuters

Raia wa
Uganda wanapiga kura leo katika uchaguzi wa rais, ambapo Rais Yoweri Museveni –
ambaye amekuwa madarakani kwa miongo minne – anawania muhula mwingine.

Shughuli ya
upigaji kura inafanyika wakati intaneti imeminywa.

Uchaguzi huu
unafanyika katika mazingira ambayo sio tofauti sana na chaguzi zilizopita hali
ya wasiwasi ikiwa imetanda na ulinzi mkali ukiimarishwa.

Rais aliye madarakani, Yoweri Museveni mwenye umri wa
miaka themanini na moja, anawania muhula wa saba baada ya kuwa madarakani kwa
zaidi ya miaka arobaini, akiwa kinyang’anyironi na wagombea wengine saba.

Mpinzani
wake mkuu, ambaye ana karibu nusu ya umri wake, ni Robert Kyagulanyi, almaarufu
Bobi Wine, ambaye anagombea urais kwa mara ya pili na kuungwa mkono sana na
wapiga kura vijana.

Waangalizi wa uchaguzi hawaruhusiwi kisheria kutoa maoni
yao kuhusu mchakato huo kupitia njia za mawasiliano zilizozoeleka au mitandao ya
kijamii, na hivyo kuzuia uchunguzi huru wa umma wa shughuli ya upigaji kura inavyoendeshwa.

Vituo vya kupigia kura vinafunguliwa saa moja asubuhi na
vitafungwa saa kumi alasiri kwa saa za eneo, huku mshindi akitarajiwa
kutangazwa ifikapo Jumamosi mchana.

Soma zaidi:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *