
Kamandi ya Marekani barani Afrika (AFRICOM) imetangaza kwamba “imepeleka vifaa muhimu vya kijeshi” nchini Nigeria, wiki chache baada ya kufanya mashambulizi ya anga katika eneo la Sokoto kulenga rasmi “Islamc State.” Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akishutumu vurugu za mara kwa mara, ambazo anadai zinawalenga Wakristo nchini humo, dai ambalo Abuja imekuwa ikikanusha vikali. Hata hivyo, utoaji huu wa silaha unaashiria kuimarisha ushirikiano wa usalama kati ya Abuja na Washington.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na ujumbe wa Africom uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii X, kupelekwa kwa vifaa hivi kunalenga kuunga mkono “operesheni zinazoendelea nchini Nigeria” na “kunasisitiza ushirikiano wa pamoja wa usalama,” hasa katika mapambano dhidi ya wanajihadi.
Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu aina ya vifaa hivi, lakini mkutano ulifanyika hivi karibuni huko San Diego, Marekani, kati ya Mkuu wa Jeshi la Anga la Nigeria na maafisa wakuu wa serikali ya Marekani, pamoja na wawakilishi kampuni ya Marekani ya Bell Textron inayotengeneza helikopta.
Majadiliano hayo yalilenga utoaji wa helikopta 12 za kivita za AH-1Z Viper ili kuimarisha uwezo wa mapigano ya angani wa jeshi la Nigeria haraka iwezekanavyo.
Ujumbe wa Nigeria ulitembelea Marekani mnamo Juni 2025 ili kujadili ununuzi wa ndege hizi za kisasa. Mkutano huu ulikuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji kati ya Abuja na Washington katika nyanja za ujasusi, mafunzo, na usaidizi wa matengenezo.
Sambamba na uwasilishaji wa vifaa uliotangazwa siku ya Jumanne, Januari 13, ujumbe wa ngazi ya juu kutoka AFRICOM ulikutana na mkurugenzi wa shirika la kupambana na dawa za kulevya nchini Nigeria huko Abuja siku hiyo, ambaye aliomba msaada katika kupata vifaa muhimu kwa usalama wa uwanja wa ndege.