MTWARA: VIONGOZI wa ngazi mbalimbali mkoani Mtwara wametakiwa kuweka mikakati mahususi kwa kushirikiana na wazazi na walezi ili kuhakikisha wanafunzi walioandikishwa elimu ya awali, msingi, sekondari na wanaoendelea wanaripoti shule.

Akizungumza wilayani Newala mkoani Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala amesema serikali imeweka bayana kuwa elimu ni bure hivyo viongozi hao wanawajibu wa kuhakikisha watoto wanapata elimu bora.

“Nitoe rai kufanyike operesheni maalumu na tuiite operesheni nenda shule kwa kuhakikisha watoto wetu wanaenda shule kwani elimu haina mbadala, “amesema Sawala.

Aidha, akiwa wilayani huo mkuu huyo wa mkoa amepata fursa ya kukagua miundombinu ya elimu katika Halmashauri ya Mji Newala pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Aidha, ukaguzi wa miundombinu hiyo ni sehemu ya ziara yake inayoendelea kwa kutembelea halmashauri zote tisa mkoani humo ili kujionea maendeleo ya miundombinu hiyo pia hali ya watoto kuripoti  shule.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *