Ukraine imetangaza hali ya hatari katika sekta ya nishati ya nchi hiyo, ikilenga zaidi Kyiv, huku mashambulizi yanayoendelea ya Urusi yakiendelea kuwaacha maelfu ya wakazi bila umeme.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Volodymyr Zelensky ameishutumu Moscow kwa kutumia kimakusudi hali ngumu ya majira ya baridi kali kama sehemu ya mkakati wake wa vita, huku halijoto ya usiku kucha huko Kyiv ikishuka hivi karibuni hadi karibu -20C.

Kauli hii inakuja wakati Rais wa Marekani Donald Trump akidai kuzuia juhudi za kufikia makubaliano ya amani ili kukomesha karibu miaka minne ya vita na Urusi.

Aliiambia Reuters siku ya Jumatano kwamba Ukraine “haiko tayari kufanya makubaliano” kuliko Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Alipoulizwa kwa nini mazungumzo ya amani bado hayajatatua mzozo huo, Trump alijibu: “Zelensky.”

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kuhudhuria Kongamano la Uchumi Duniani nchini Uswisi wiki ijayo, ingawa Trump alipendekeza hakuna mipango rasmi iliyopangwa ili wakutane.

Katika wiki za hivi karibuni, mashambulizi ya Urusi dhidi ya Kyiv yameacha maelfu ya nyumba bila umeme, joto, na maji ya bomba. Baada ya usiku wa mmashambulizi makali ya makombora na ndege zisizo na rubani wiki iliyopita, 70% ya mji mkuu ulikuwa hauana umeme kwa saa kadhaa.

Kufuatia mkutano wa dharura wa baraza la mawaziri siku ya Jumatano, Zelensky alitangaza kuanzishwa kwa timu ya dharura ya operesheni ya saa 24 kwa siku, ili kushughulikia uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Urusi na hali mbaya ya hewa.

Alisema hatua mpya zitajumuisha ununuzi wa vifaa muhimu vya nishati na rasilimali kutoka nje ya nchi ili kubadilisha mitambo iliyoharibika.

“Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza – Waziri wa Nishati wa Ukraine amepewa jukumu la kusimamia kazi ya kuwasaidia watu na jamii chini ya hali hizi,” ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Pia aliamuru ongezeko la idadi ya vituo vya usaidizi wa dharura kuzunguka Kyiv ili kutoa joto na umeme kwa wakazi, hatua ambayo inaweza kusababisha kulegezwa kwa sheria ya kutotoka nje usiku wa manane katika mji mkuu.

Wiki iliyopita, maafisa wa Ukraine walisema kwamba zaidi ya watu milioni moja kusini mashariki mwa Ukraine walitumia saa nyingi bila kupasha joto na maji kutokana na mashambulizi ya anga ya Urusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *