Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini, Angie Motshekg, ameagiza uchunguzi kufanyika kuhusu ripoti ya Iran kushiriki katika mazoezi ya wanajeshi wa majini, kinyume na maagizo ya rais.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huo unakwenda kufanyika baada ya Marekani kukosoa vikali mazoezi hayo ya wiki iliopita, yaliojuluisha meli za kivita kutoka China, Iran, urusi na nchi ya falme za Kiarabu katika eneo la bahari karibu na mji wa Cape Town.

Vyombo vya habari nchini Afrika kusini vimeripoti kwamba rais Cyril Ramaphosa amemuagiza waziri wa ulinzi, kuziondoa meli tatu za kivita za Iran kwenye mazoezi hayo yanayofanyika wakati huu serikali ya Iran ikiendeleza msako dhidi ya waandamanaji.

Bodi ya uchunguzi inatarajiwa kuchunguza ikiwa maagizo ya rais yanaweza kuwa yalipotoshwa au yalipuuzwa.

Kulingana na jeshi, mazoezi hayo ya muungano wa nchi za BRICS yanayoongozwa na China, yanalenga kutoa hakikishi kwa shughuli za kiuchumu za baharini.

Hata hivyo haijabainika wazi ni kwa kiwango gani Iran imeshiriki kwenye mazoei hayo ya kijeshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *