Matokeo ya awali ya uchaguzi nchini Uganda 2026, yanaonesha Rais Yoweri Museveni wa NRM aliye madarakani anaongoza kwa asilimia zaidi ya 60 ya kura zilizopigwa.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Uganda Jaji Simon Byabakama, alisema matokeo hayo yamezingatia vituo 133 vya kupiga kura yaliowakilisha asilimia 0.26 ya jumla ya kura zilizopigwa.
Byabakama alithibitisha kuwa taarifa zingine juu ya uchaguzi zitatolewa Ijumaa, saa tatu asubuhi wakati matokeo zaidi yanaendelea kuwasilishwa katika kituo kikuu cha kuhesabu kura kilichoko eneo la Wakiso.
Awali, Jaji Byabakama alisema kuwa siku ya uchaguzi ilikwenda vizuri ingawa uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto za hitilafu ya kimitambo ikiwa ni pamoja na mashine za kupiga kura zilizoshindwa kufanyakazi na kulazimisha shughuli ya upigaji kura kuendelea kwa njia ya kawaida.
Mgombea wa upinzani Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) amedai uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu.