
Rais wa Tanzania amezungumza kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa mwezi Oktoba uliopingwa kuhusu kuzimwa kwa mtandao wa intaneti kulikosababisha nchi hiyo kuinfia katiak sintofahamu kwa siku sita, huku Tanzania ikikumbwa na vurugu mbaya zaidi baada ya uchaguzi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais Samia Suluhu Hassan alielezea “masikitiko” yake siku ya Alhamisi kwa wanadiplomasia na raia wa kigeni wanaoishi nchini humo, akiwahakikishia kwamba serikali itafanya kila linalowezekana kuzuia hali kama hiyo kutokea tena.
Samia Suluhu Hassan alishinda uchaguzi wa mwezi Oktoba kwa zaidi ya 97% ya kura, baada ya wagombea kutoka vyama viwili vikuu vya upinzani kupigwa marufuku na kiongozi mkuu wa upinzani kubaki gerezani, akituhumiwa kwa uhaini.
Ghasia zilizuka siku ya uchaguzi na kuendelea kwa siku kadhaa, huku ufikiaji wa intaneti ukikatizwa wakati ukandamizaji wa polisi ukisababisha vifo vya mamia ya watu, kulingana na mashirika ya haki za binadamu.
Rais Samia Suluhu Hassan alihusisha vurugu hizo kwa raia wa kiwageni na kuwasamehe mamia ya vijana waliokamatwa, akidai kwamba walitenda chini ya shinikizo la wenzao.
Akihutubia mabalozi, makamishna wakuu, na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa huko Dodoma, mji mkuu wa Tanzania, siku ya Alhamisi, alitaka kuwahakikishia kuhusu usalama wao, akisema kwamba serikali itaendelea kuwa macho ili kuzuia machafuko kama hayo yasijirudie tena.
“Kwa washirika wetu katika kikosi cha wanadiplomasia na kwa wakazi wa kigeni nchini Tanzania, natoa pole zangu za dhati kwa kutokuwa na uhakika, vikwazo vya huduma, na kukatika kwa mtandao wa intaneti, yaani hali mbaya ambayo mliopitia,” alisema.
Rais Samia Suluhu Hassan alitetea serikali yake, akidai kwamba hatua zilizochukuliwa zililenga kuhifadhi utaratibu wa kikatiba na kuwalinda raia.
“Ninawahakikishia kwamba tutaendelea kuwa macho ili kuhakikisha usalama wenu na kuzuia matukio kama hayo yasijirudie tena,” rais aliwaambia wanadiplomasia siku ya Alhamisi.
Tangu uchaguzi wa mwezi Oktoba, Tanzania imeanzisha tume ya uchunguzi kuchunguza vurugu zilizosababisha vifo vya mamia na kusababisha uharibifu wa mali wa mamilioni ya shilingi katika nchi ambayo ilikuwa imeshuhudia amani kwa miongo kadhaa.
Waangalizi wa kigeni wamesema kwamba uchaguzi huo haukufikia viwango vya kidemokrasia kwa sababu watu muhimu wa upinzani walizuiwa kushiriki.