Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeendelea kung’ara katika utoaji wa huduma za matibabu ya mifupa katika ukanda wa nchi zinazoendelea na zinazopokea ufadhili wa vifaa tiba vya upasuaji wa mivunjiko ya mifupa kutoka shirika lisilo la kiserikali la nchini Marekani, Surgical Implant Generation Network (SIGN).
Kupitia tathmini ya kimataifa iliyotolewa jana Januari 15, MOI imeshika nafasi ya pili kati ya hospitali 450 duniani kote zinazoshirikiana na SIGN.
SIGN ni shirika ambalo kwa zaidi ya miaka 25 limekuwa likiratibu na kufadhili vipandikizi pamoja na vifaa vya upasuaji kwa nchi zinazoendelea, kwa lengo la kuboresha huduma za matibabu ya mifupa duniani.
Mhariri @moseskwindi