
Wasuluhishi na wawezeshaji wa mchakato wa kupata amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na katika eneo la Maziwa Makuu, wapo jijni Lome nchini Togo ambako watahudhuria kikao cha pamoja siku ya Jumamosi kujadili mwenendo wa mchakato wa amani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Lengo la mkutano huo ni kuimarisha ushirikiano kati ya wadau wote wanaohusika kwenye mchakato wa kusaidia kuleta amani Mashariki mwa DRC lakini na kuendeleza mazungumzo kati ya pande zinazokinzana lakini pia kuthathmini utekelezwaji wa makubaliano yaliyoafikiwa kama ule wa Washington.
Mwenyeji wa mkutano huo ni rais wa Togo Faure Gnassingbé, mpatanishi wa Umoja wa Afrika, ambaye siku ya Alhamisi alikutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf.
Ujumbe kutoka Marekani, Qatar, DRC, Rwanda pamoja na marais wa zamani Olusegun Obasanajo, Uhuru Kenyatta, Catherine Samba-Panza, Mokgweetsi Masisi na Sahle-Work Zewde ambao ni wawezeshaji watakuwepo pia kwenye mkutano huo.
Michakato ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, na Kusini mwa Afrika SADC, iliunganishwa na kuwaweka wawezesheaji hao pamoja, ili kumsaidia mpatanishi wa Umoja wa Afrika kupata suluhu ya kudumu ya utovu wa usalama na siasa Mashariki mwa DRC na eneo la Maziwa Makuu.