
Watu karibu Milioni 55 katika nchi za Afrika Magharibi na Kati, wanakabiliwana uhaba wa chakula, hali ambayo inatarajiwa kuendelea kushuhudiwa mwaka huu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Nigeria ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na changamoto hiyo, ambapo wakaazi wa jimbo la Borno wapo katika hali mbaya, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa.
Ukosefu wa usalama katika ukanda huo, na kupunguzwa kwa viwango vya misaada ya kibinadamu ni miongoni mwa sababu za nchi hiyo kukabiliwa baa la njaa.
Shirika la Mpango wa chakula duniani WFP limesema iwapo hali haitabadilika kwa wahisani kujitokeza, hali itakuwa mbaya zaidi kati ya mwezi Juni na Agosti.
Aidha, WFP inasema idadi ya watu wanaotafuta misaada ya kibinadamu hasa chakula imeongezeka kwa Milioni tatu, tangu mwaka 2020.