Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi, Uwenezi na Mafunzo, Ndugu Kenani Labani Kihongosi amesema kuwa CCM ni chama cha kimaendeleo na chama cha kijamii, kinachojengwa juu ya misingi ya amani, umoja, mshikamano na kulinda utu wa Mtanzania, na kwamba misingi hiyo ndiyo iliyokiwezesha chama kukiongoza Taifa kwa muda mrefu kwa uthabiti na amani.