Tume ya Uchaguzi nchini Uganda, siku ya Jumamosi imemtangaza rais Yoweri Museveni, mwenye umri wa miaka 81, mshindi wa uchaguzi wa urais  uliofanyika siku ya Alhamisi kwa kupata asilimia 71.65 ya kura, huku mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine akiwa wa pili kwa kupata asilimia 24.72 ya kura.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Simon Byamukama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Uganda, ametangaza Museveni mshindi kwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa.

“Tume inamtangaza mgombea Museveni kama mshindi wa uchaguzi wa urais kwa miaka mitano itayo” alisema Byamukama.

Ushindi huu unampa Museveni ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 40, nafasi ya kuendelea kuongoza nchi hiyo kwa miaka mingine mitano ijayo.

Hata hivyo, mpinzani wake Mkuu Bobi Wine ambaye amekataa kutambua matokeo hayo, na kuwataka raia wa Uganda kuandamana kwa amani, kudai kile alichosema ni  kudai ushindi wao.

“Tunakata kile kilichotangazwa na Bwana Byamukama. Matokeo hayo ni bandia, hayaoneshi kilichotokea kwenye vituo vya kupigia kura na fomu za kuonesha matokeo” Alisema.

“Tunawaomba raia wa Uganda wakatae matokeo hayo, na bila kutumia fujo waandamane na kukataa jitihada zozote za kunyamazisha sauti zao, na kudai matokeo sahihi yatangazwe” aliongeza  kupitia  mkanda wa video uliochapishwa kwenye ukurasa wake wa kijamii wa X.

Bobi Wine mwenye umri wa miaka 43, hayafamiki yuko wapi, baada ya kudai kuwa ametoroka nyumbani kwake kuanzia Ijumaa usiku, baada ya kuwepo kwa mpango wa jeshi na polisi kumkamata, madai ambayo vyombo vya usalama nchini Uganda, vimekanusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *