Rais wa Shirikisho la Soka Afrika(CAF), Dkt Patrice Motsepe amefuta mashindano yanayohusu wachezaji wanaocheza Ligi za ndani (CHAN), akidai yanagharimu kiasi kikubwa cha fedha.
Motsepe ametoa kauli hiyo kupitia mkutano wake na waandishi wa habari jijini Rabat, Morocco.
”Kazi yetu ni kufanya maamuzi yenye maslahi kwa soka la Afrika. CHAN ni mashindano ambayo yanatufanya tupoteze fedha,” amesema.
Motsepe ameongeza kuwa CAF ilihitaji kufikiria upya vipaumbele vyake.
Ikumbukwe hilo linakuja baada ya mabadiliko ya michuano ya AFCON kutoka kuchezwa kila baada ya miaka miwili na sasa ikiwa ni kila baada ya. miaka minne.
Mashindano ya CHAN mara ya mwisho yalifanyika Afrika Mashariki chini ya nchi tatu, Kenya, Tanzania na Uganda, huku ubingwa ukichukuliwa na Morocco.
#StarTvUpdate