Shirikisho la soka la Senegal linaishutumu Morocco kwa majaribio ya makusudi ya kuhujumu Fainali ya AFCON kati ya timu hizo mbili iliyopangwa Jumapili, Januari 18.
Katika taarifa yenye maneno makali, Senegal ilidai msururu wa vikwazo vilivyopangwa hasa ukosefu wa usalama wa kutosha walipofika kwenye kituo cha gari Moshi cha Rabat na kupata matatizo makubwa ya kukata tiketi, kuingia Uwanjani na hata hoteli.
Senegal sasa inatoa wito kwa CAF na Kamati ya Mpaandalizi ya ndani kuingilia kati, kushughulikia na kuhakikisha usawa, usalama sahihi kwa wote.