Simba SC imemtambulisha mchezaji mpya, Lebasse Guaye raia wa Senegal kutoka klabu ya Teungueth ya Senegal.

Guaye anatoka taifa moja na staa wa zamani wa Liverpool, Sadio Mane kwa maana wote ni raia wa Senegal.

Kama haitoshi nyota huyo ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili pia anacheza nafasi ya winga kama ilivyo kwa Sadio Mane.

Mkali huyo mara ya mwisho alionekana ardhi ya Tanzania akiwa na timu ya Taifa ya Senegal kwenye michuano ya CHAN kundi ambalo mechi zake zilichezwa Uwanja wa New Amaan, Zanzibar huku akibuka mchezaji bora wa mechi dhidi ya Nigeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *