Rais wa Tanzania Samia Suluhu kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa Oktoba mwaka uliopita, amezungumzia hatua ya serikali yake kuzima mtandao wa intaneti wakati na baada ya uchaguzi huo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Alhamisi ya wiki hii, Rais Samia aliwaomba msamaha wanadiplomasia na raia wote wa kigeni wanaoishi nchini Tanzania kutokana na kilichotekea wakati huo, akiahidi kuwa serikali yake itachukua hatua kuhakikisha kilichotokea hakijirudii tena.

Hassan alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba kwa asililia 97, uchaguzi ambao wapinzani wake wakuu walizuiliwa kushikiri, katibu mkuu wa chama kikuu cha upinzani Tundu Lissu aikisalia gerezani kwa tuhuma za uhaini.

Vurugu zilizuka wakati wa uchaguzi, mtandao wa intaneti ukizimwa, mamia ya raia wakiripotiwa kuuawa na polisi kwa mujibu wa mashirika ya kiraia.

Polisi wa Tanzania wakati wa oparesheni dhidi ya waandamanaji katika mpaka wa Kenya na Tanzania.
Polisi wa Tanzania wakati wa oparesheni dhidi ya waandamanaji katika mpaka wa Kenya na Tanzania. REUTERS – Thomas Mukoya

Hassan aliwatuhumu wageni kwa vurugu hizo za wakati wa uchaguzi, akitangaza msamaha kwa vijana waliokamatwa kwa kuhusishwa na vurugu hizo akisema walilazimishwa kushiriki maandamano dhidi ya serikali.

Wakati akizungumza na mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa jijini Dodoma Alhamisi ya wiki hii, Rais Samia aliwahakikisha usalama wao na kwamba kilichotokea wakai huo hakitajirudia tena.

Kwa washirika wetu katika sekta ya kidiplomasia na wageni wanaoishi hapa Tanzania, ninawapa pole Kwa kilichotokea, changamoto za kuzimwa na kutopatikana kwa intaneti mlizopitia,” alisema Rais Samia.

Hassan alitetea uongozi wake, akisema hatua hizo zilichukuliwa ili kulinda utaratibu wa kikatiba na kulinda raia.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. via REUTERS – PRESIDENTIAL PRESS UNIT

“Ninawahakikishia kuwa tutaendelea kuwa macho ili kuhakikisha usalama wenu na kuzuia kujirudia kwa matukio kama hayo,” rais aliwaambia wanadiplomasia siku ya Alhamisi.

Tangu mwezi Oktoba, serikali ya Tanzania imeunda tume ya uchunguzi kuchunguza vurugu zilizotokea na kusababisha vifo vya mamia ya watu pamoja na uharibifu wa meli yenye mamilioni ya pesa.

Waangalizi wa kimataifa walisema uchaguzi huo hakukidhidi viwango vya kidemokrasia kutokana na hatua ya kuzuiliwa kwa wapinzani wakuu wa Rais Samia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *