Tume ya uchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025 itakutana na kuwasikiliza wananachi Wiilaya ya Ilala.
Taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo imesema kuwa Tume hiyo inatarajiwa kuwa wilayani humo Jumatatu, Januari 19,2026.
Kwa mujibu wa Mpogolo, Tume itakutana na kuwasikiliza wananachi walioathirika kwa kufiwa na ndugu, kujeruhiwa, kuharibiwa na kuibiwa mali zao.
“Muda ni kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa Karimjee. Wakazi wote wa Ilala mnakaribishwa,” amesisitiza mkuu huyo wa wilaya.