
Katika mkanda wa video uliochapishwa kwenye mtandao wa X, mtoto wa kiume wa Bobi Wine- Solomon Kampala amedai kuwa babake alifanikiwa kuwakwepa wanajeshi wa nchi hiyo wakati walipodaiwa kuvamia makazi yao.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jeshi nchini humo limekanusha ripoti za chama cha Bobi Wine kuwa kiongozi wao alichukuliwa nyumbani kwake kwa ndege ya kijeshi na kupelekwa kusikojulikana.
Chama cha Wine National Unity Platform (NUP) usiku wa Ijumaa kilidai kuwa kiongozi wao alichukuliwa kwa nguvu na kusafirishwa kwa helikopta ya kijeshi kutoka katika makazi yake na kupelekwa kusikojulikana.
Katika hatua nyengine, msemaji wa polisi nchini Uganda Kituuma Rusoke amesema Bobi Wine yupo nyumbani kwake na yupo huru kutembea.
Wine amedai kuwepo kwa udaganyifu mkubwa katika uchaguzi wa urais wa Januari 15 mwaka huu, uchaguzi uliofanyika mtandao wa intaneti ukiwa umezimwa. Aidha amewataka wafuasi wake kuandamana.
Alhamisi ya wiki hii, chama chake pia kilidai kuwa kiongozi wao alikuwa anazuiliwa nyumbani kwake.
Rais Museveni anatarajiwa kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo, ambapo hadi kufikia sasa, anaoongozwa kwa zaidi ya asilimia 70 ya matokeo ya kura kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.