Waziri wa Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, amewataka watumishi wa umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida Fund kama njia ya kujipatia uhuru wa kifedha kabla na baada ya kustaafu.

Akifungua mkutano mkuu wa tatu wa mfuko huo jijini Dar es Salaam, Ridhiwani amesema bado hajaridhishwa na watumishi 12,000 pekee waliowekeza, na akahimiza uongozi wa Faida Fund kubuni mikakati zaidi ya kuwavutia wawekezaji wengi ili kuongeza tija na ustawi wa watumishi nchini.

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *