
Kundi la AFC/M23 hatimaye lilitangaza siku ya kuondoka kabisa kutoka katika jiji hilo. Siku ya Jumamosi alaasiri, safu za wapiganaji wa AFC/M23 zilionekana zikiondoka Uvira.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Watu waliovaa mavazi ya kijeshi, silaha zikiwa zimewekwa mabegani mwao, kofia za chuma vichwani mwao. Walielekea upande wa kaskazini wa kutokea mji. Baadhi wakitembea kwa miguu, wengine wakichukuliwa na malori yaliyowekwa kwenye njia ya kutokea. Kulingana na vyanzo vya RFI kutoka mjini hapo, kulikuwa na takriban wapiganaji 300, wote wakiwa na silaha. Huku ni kile AFC/M23 inachoita “kitengo cha uchunguzi na ufuatiliaji.”
Wanajeshi hao waliondoka wakazi ambao walikuwa wamekusanyika kando ya barabara kuu, wakishuhudia. Raia walikuwa na wasiwasi tangu asubuhi, kufuatia milio ya risasi iliyosikika katika vilima vinavyoelekea Uvira.
Kulingana na taarifa zetu, wapiganaji wa Wazalendo, pamoja na vikosi vya Jeshi la Kongo (FARDC), wamepia kambi kwenye umbali wa kilomita chache kutoka jiji hilo.
Kwa upande wake, AFC/M23 inabainisha kuiweka Uvira “chini ya uangalizi na jukumu kamili la jumuiya ya kimataifa” na inasema sasa inakataa jukumu lote la kulinda usalama wa jiji hilo lenye wakazi wake wapatao 500,000. Bado haijabainika ikiwa, na lini, FARDC itaamua kurudi na kuchukua tena udhibiti wa jiji la Uvira.
Kufuatia shinikizo kutoka Marekani, AFC/M23 ilitangaza kuondoa wanajeshi wake kutoka Uvira, jiji la pili kwa ukubwa katika jimbo la Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kindi hili lilichukua udhibiti wa jiji mapema mwezi Desemba. Wapiganaji wengi na vifaa vyao waliondoka mji wa Uvira, lakini wapiganaji wadogo wa AFC/M23 na viongozi tawala kutoka kundi hilo waliendelea kubaki katika mji huo.