Mbunge wa Viti Maalum, Halima Idd Nassor, amefariki dunia leo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Dar es Salaam wakati alipokuwa akitibiwa.
“Kwa masikitiko makubwa, natangaza kifo cha Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Halima Idd Nassoro, Natoa pole kwa Waheshimiwa Wabunge wote, familia ya Marehemu, ndugu, jamaa na marafiki, Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu.
Kwa mujibu wa ofisi ya Bunge, mipango ya mazishi na taarifa Zaidi zitaendelea kutolewa.
#AzamTVUpdates