Mbunge wa Viti Maalumu, CCM – kundi la wafanyakazi, Halima Iddi Nassor amefariki dunia.
Taarifa ya Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu imesema Halima amefikwa na umauti leo Jumapili, Januari 18,2026.
Halima alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
Halima alikuwa pia Mwenyekiti wa Kamati ya Mapambano ya Ukatili wa Kijinsia Mkoa wa Mwanza kupitia Umoja wa Wanawake (UWT).
#StarTvUpdate