Sierra Leone, leo Jumapili, Januari 18, inazindua Siku ya kitaifa ya ukumbusho. Tarehe hii imetangazwa na Rais Julius Maada Bio kutekeleza pendekezo muhimu la Tume ya Ukweli na Maridhiano. Mamlaka inawataka Wasierra Leone kushiriki kama kitendo cha pamoja cha ukumbusho na mshikamano—“kutafakari yaliyopita” na kuchukua hatua “za dhamiri” na “za kizalendo” ili “kufanya yaliyo sawa kwa Mama Salone.” 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Januari 18, 2002, iliashiria mwisho rasmi wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka kumi na moja vilivyoanza mwaka wa 1991—mzozo ambao makovu yake yanabaki mabichi kwa maelfu ya manusura.

Yote yalianza Machi 23, 1991, mashariki mwa nchi: Vuguvugu la waasi la RUF (Revolutionary United Front) lilianzisha mashambulizi, ikidai kutaka “kuikomboa” Sierra Leone kutoka kwa mfumo uliojaa ufisadi, dhuluma, na kupuuzwa kwa sehemu kubwa ya watu. Lakini haraka sana, uasi huo ulichochea vitisho: vijiji vilichomwa moto, raia walilengwa, watoto waliandikishwa jeshini, ukatili wa kijinsia ulitekelezwa, na ukeketaji ulifanywa.

Katika eneo la Kono, almasi iligeuka kuwa damu ya vita: udhibiti wa maeneo ya uchimbaji madini ulifadhili mapigano na kuchochea mapambano kati ya makundi. Vita vilirindima katii ya makundi yaliyo hasimu yaliyojitenga, Vita vilipamba moto katikati ya hali machafuko ya kisiasa na mapinduzi ya kijeshi.

Katika kumbukumu, tarehe moja inabaki kuwa chanzo cha mshtuko: Januari 6, 1999, wakati vurugu zilipofika Freetown, kitovu cha kisiasa na kiuchumi cha nchi.

Baada ya makubaliano kadhaa ya amani yaliyoshindwa, kuwasili kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa, na kupokonywa silaha polepole kwa wapiganaji, vita viliisha rasmi mwaka wa 2002. Kisha ikaja Tume ya Ukweli na Maridhiano na Mahakama Maalum—lakini kwa waathiriwa wengi, haki bado haijakamilika.

Na hiyo ndiyo hoja nzima ya Siku hii ya kitaifa ya ukumbusho: kuelewa kilichosababisha machafuko, ili kuepuka kutumbukia tena ndani yake.

“Kusahau ni hatari.” Abass Sesay alikuwa na umri wa miaka mitatu wakati waasi waliposhambulia kijiji chake. Bibi yake aliuawa, na akapoteza mguu. Kwake, Siku hii ya Ukumbusho ni muhimu: “Kusahau ni hatari.”

Nilikuwa na umri wa miaka mitatu wakati waasi waliposhambulia jamii yangu. Walitoka msituni, wakichoma nyumba na kuwapiga risasi watu.

Mimi na bibi yangu tulijificha kwenye chumba cha chini. Nilikuwa nikilia—sikuwa nimekula siku nzima—na watu waliogopa waasi wangetusikia. Kwa hivyo mama yangu alitoka kwenda kupata kitu cha kula. Bibi yangu alimfuata, akinibeba mgongoni.

Waasi waliwaona. Mama yangu aliingiwa na hofu, na bibi yangu pia. Walikimbia, lakini  waasi wakaaza kufyatuliana risasi na vikosi vya ulinzi na usalama. Risasi ilimpata bibi yangu: aliuawa. Mimi pia nilipigwa, kichwani na mkononi. Mkono wangu ulizidi kuwa mbaya kwa siku baada ya , na nilipofika hospitalini, niilikuwa nimechelewa. Madaktari walilazimika kuukata.”

Ndiyo maana Siku ya Ukumbusho ni muhimu: kukumbuka vita na athari zake—vifo, mshtuko, kile kilichoivuruga nchi yetu. Hata leo, tunajaribu kujenga upya kile kilichovunjika. Kusahau ni hatari: tukisahau sababu za vita, tunaweza kurudi katika vita hivyo.

SCSL ni ya kipekee kwa kuwa inasimamia haki mahali; hii inawezesha raia wa Sierra Leone kushuhudia kesi na hukumu za washtakiwa wakuu wa mahakama. Hata hivyo, wengi wanakosoa kiputo cha teknolojia ya hali ya juu ambacho mahakama inawakilisha, pamoja na msafara wake wa wageni wenye mishahara mikubwa. Zaidi ya kauli zenye nia njema, wengi pia wanalaani ukosefu wa ushiriki katika kesi hizo na ushiriki wa umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *