.

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Klabu ya Chelsea iko tayari kulipa euro 50m (£43.3m) kwa mlinzi wa Ufaransa Jeremy Jacquet, 20, lakini Rennes wanataka zaidi ya euro 60m (£52m). (RMC Sport – kwa Kifaransa)

Napoli huenda ikamsajili mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland Evan Ferguson, 21, ambaye yuko Roma kwa mkopo kutoka Brighton, ikiwa winga wa Uholanzi Noa Lang, 26, ataondoka mwezi huu. (Corriere dello Sport – kwa Kiitaliano)

Uongozi wa Tottenham unatarajiwa kukutana leo Jumapili kujadili mustakabali wa meneja Thomas Frank baada ya klabu hiyo kushindwa Jumamosi dhidi ya West Ham.(Independent)

Bournemouth inajadiliana na klabu ya Lazio kuhusu mkataba wa mkopo kwa kipa wa Ugiriki Christos Mandas, 24. (Sky Sports)

Newcastle imewasilisha dau la kumsajili mlinzi wa Uholanzi na Inter Milan Stefan de Vrij, 33. (Football Insider)

Aston Villa imefanya mazungumzo na Club Brugge kuhusu usajili wa Raphael Onyedika, 24, lakini Galatasaray inaongoza mbio za kumsajili kiungo huyo wa Nigeria. (Sacha Tavolieri),

Arsenal wanamuwania mchezaji wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 22 na beki wa Eintracht Frankfurt Nathaniel Brown na kiungo wa kati wa Sporting wa Ivory Coast Ousmane Diomande, 22. (Caught offside).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *