Senegal wameibuka mabingwa wa michuano ya soka kwa mataifa ya Afrika AFCON baada ya kuwafunga wenyeji Morocco bao 1-0 katika mechi ya kusisimua ya fainaili iliyopigwa usiku wa kuamkia Jumatatu jijini Rabat.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Bao la kiungo wa Kati Pape Gueye katika dakika ya 94, kimeipa Senegal ubingwa wa AFCON mbele ya maelfu ya mashabiki wa Morocco.

Ubingwa huu ulikuja  baada ya Morocco kushindwa kufungwa penalti kupitia mchezaji wake Brahim Diaz.

Uamuzi wa mwamuzi kutoka DRC Jean-Jacques Ndala kuipa Morocco penalti, ulisababisha kizaaza uwanjani, baada ya kocha wa Senegal Pape Bouna Thiaw kuamuru wachezaji kutoka uwanjani, kama kitendo cha kuonesha kuonewa.

Hata hivyo, jitihada za mshambuliaji Sadio Mane, zilifanikisha kuwarejesha uwanjani na wakaendelea na mchuano huo baada ya kucheleweshwa kwa dakika 14.

“Nilishauriana na watu mbalimbali, wakanishauri tumalize mchezo. Hii ilinisukuma kuwashawishi wachezaji wenzangu warejee uwanjani,” alisema Mane baada ya mchuano huo.

Ushindi wa Senegal, umesherehekewa usiku kucha nchini Senegal hasa jijini Dakar.

Rais Bassirou Diomaye Faye ametangaza Jumatatu siku ya mapumziko baada ya ushindi wa Senegal.

“Tunatoa fursa kwa wananchi washerehekee ushindi huu muhimu. Tumejipanga vizuri kuikaribisha timu yetu,” alisema baada ya ushindi huo.

Hii ni mara ya  pili kwa Senegal kushinda taji la AFCON mara kwanza ilikuwa ni mwaka 2021.

Baada ya Morocco, sasa maandalizi ya Kenya, Uganda na Tanzania kuwa wenyeji wa michuano hii mwaka 2027 yameanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *