
Baraza la Katiba nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, limetangaza mnamo Januari 19, 2026, kuchaguliwa tena kwa Rais Faustin-Archange Touadéra kwa muhula wa tatu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Baraza la Katiba limeamua kuwa haikubaliki kwa misingi ya utaratibu rufaa ya kufuta uchaguzi huo iliyowasilishwa na mpinzani wake mkuu, Anicet-Georges Dologuélé.
Kulingana na matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa Desemba 28, Faustin-Archange Touadéra alipata 77.9% ya kura dhidi ya 13.5% ya kura alizopata mgombea wa upinzani, ambaye alilaani udanganyifu mara kadhaa. Idadi ya wapiga kura ilirekebishwa hadi 64.42%.
Mapema mwezi Januari Mamlaka ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitangaza kwamba Rais Faustin-Archange Touadéra alichaguliwa tena kwa asilimia 76.15 ya kura. Sehemu ya upinzani ilisusia uchaguzi huo.
Faustin-Archange Touadéra ambaye alichaguliwa mwaka wa 2016 na kisha kuchaguliwa tena mwaka wa 2020 katika uchaguzi uliojaa tuhuma za udanganyifu, anakosolewa kwa kupitisha Katiba mpya mwaka wa 2023 iliyomruhusu kusalia madarakani.