Shuhudia namna polisi wa Guatemala ‘walivyomchomoa gerezani’ anayedaiwa kuwa kiongozi wa genge la kihalifu la Barrio 18, ajulikanaye kwa jina na Aldo Dupie, maarufu kwa jina la Mbwa Mwitu.

Aldo amekamatwa wakati wa operesheni ya kurejesha udhibiti wa gereza lenye usalama wa juu la Renovacion I, lililopo Escuintla, takriban kilomita 75 kusini mwa mji wa Guatemala.

Genge la Barrio 18 pamoja na hasimu wake Mara Salvatrucha (MS-13) wanalaumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya, wizi, na vitendo vya uhalifu vinavyoikumba nchi hiyo.

Kukamatwa kwa kiongozi huyo kunatarajiwa kupunguza ushawishi wa genge hilo, kudhibiti vurugu ndani ya gereza, na kuchangia kudumisha amani na usalama nchini Guatemala.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *